Friday, July 19, 2024

MAOMBI YA MACHOZI NI YAPI NA HUTENDA NINI MAISHANI MWETU? Pastor Godlove Indiael


 


Pointi ya 2

Maombi haya Yana uwezo wa kutafuta hata vile vilivyojificha na kuharibika maishani mwako vionekane tena.

Lazaro alitengwa na nduguze baada ya kufa, walim huuwona hafai tena maana ameoza na ananuka.

Yesu akatokea kumtafuta maana ana vitu vya utukufu wa Mungu ndani mwake.

Tambua vitu venye utukufu wa Mungu vikidhihirishwa kwako lazima ulimwengu wako wa roho uruhusu wewe kutafutwa na Mungu.

Pointi ya 3

Maombi ya machozi yana nguvu ya kuvuta vitu vilikojificha na kutokea tena maishani mwako.

Lazaro Yesu anamwita njoo huku nje.

Mwana wa Mungu unaweza kuniuliza umejuaje hili Mch Godlove.

Kuna uhusiano mkubwa Sana Kati ya vilivyojificha na vilivyopo nje vitokee.

Yesu anachofanya ni kuitumia nguvu ya kuita kwa machozi kilichojificha kaburini kiitwacho Lazaro.

Natamani Leo na wewe uite chochote chako kilichojificha katika ulimwengu wa roho kwa Jina la Yesu Kristo .

Yesu alimwita Lazaro nawe ita wala usichoke nacho kitatokea kwa Jina la Yesu .

0 comments: