KUOMBA KWA MACHOZI NI KUOMBA KWA NAMNA GANI?
Point ya 1.KUOMBA KWA KUOMBOLEZA (KWA MZIGO).
Ayubu 7:11
11 Kwa hiyo sitakizuia kinywa changu; Nitanena kwa mateso ya roho yangu; Nitalia kwa uchungu wa nafsi yangu.
Ayubu 10:1
1 Nafsi yangu inachoka na maisha yangu; Sitajizuia na kuugua kwangu; Nitanena kwa uchungu wa roho yangu.
“Rudi, ukamwambie Hezekia, mkuu wa watu wangu, Bwana, Mungu wa Daudi baba yako asema hivi, Nimeyasikia maombi yako, na kuyaona machozi yako; tazama, nitakuponya; siku ya tatu utapanda nyumbani kwa Bwana.”
2 Wafalme 20:5
“Tena Esta akasema na mfalme mara ya pili, akaanguka miguuni pake, akamsihi kwa machozi ayaondoe madhara ya Hamani, Mwagagi, na shauri.” alilowafanyia Wayahudi
Esta 8:3
“Machozi yangu yamekuwa chakula changu mchana na usiku, Pindi wanaponiambia mchana kutwa, Yuko wapi Mungu wako.” — Zaburi 42:3
Maombi ya machozi ni maombi ya kuomba kwa kumaanisha huku ukionyesha Nia yako kabisa (uhitaji wako) kabisa wa kupata toka kwa Mungu.
Biblia inatuonyesha hao watumishi wa Mungu katika vitabu tulivyo Soma hapo wanaonyesha uhitaji wao kamili mbele za Mungu ni wa namna gani.
Uhitaji unazaliwa na vitu vitatu vikuu:
1.Nia (shauku/msukumo)
2.Utayari
3.Msimamo wa mhitaji.
Maombi ya machozi yanaonyesha ulichobeba ni nini katika ulimwengu wa roho.
Kumbuka matokeo ya maombi ya kweli ni uponyaji.
0 comments: