Point ya 2. KUOMBA KWA SADAKA.
Kuna maombi ya kuomba kwa SADAKA.
1 Samweli 1:11
11 Akaweka nadhiri, akasema, Ee Bwana wa majeshi, ikiwa wewe utaliangalia teso la mjakazi wako, na kunikumbuka, wala usinisahau mimi mjakazi wako, na kunipa mimi mjakazi wako mtoto mume, ndipo mimi nitakapompa Bwana huyo mtoto siku zote za maisha yake, wala wembe hautamfikilia kichwani kamwe.
“Ndipo Samweli akatwaa mwana-kondoo mchanga, akamtolea Bwana sadaka ya kuteketezwa nzima; Samweli akamlilia Bwana kwa ajili ya Israeli; Bwana akamwitikia.”
1 Samweli 7:9
Ana anamwomba samwel kwa SADAKA.
Maombi haya ni maalumu ya kufungua na kuachilia vitu vilivyoshikilia katika ulimwengu wa roho viachilie.
Ana anaambatanisha maombi yake na sadaka ili Samwel afunguliwe alipo na ampokee.
Mfalme Daudi alipozungukwa na madui zake pande zote alichukua sadaka akaenda nayo madhabahuni kwa Mungu kwa Furaha na kilichotokea baada ya kutoa sadaka yake hao maadui zake MUNGU aliwaweka chini ya mkono wake .
Zaburi 27:2-3,6.
Kuomba kwa sadaka kunaleta•
•Mlango maalum wa kupokea
•Neema kuu ya kusikika ipasavyo mbele zake MUNGU
•Kujulikana na kutambulika kipekee mbele za MUNGU
Je, wewe unafanyaje?, Ana aliachilia sadaka yake na maombi Samwel akatokea.
Je, wewe umeambatanisha nini ili kitokee unachokingojea kwako wewe?
0 comments: