Thursday, July 18, 2024

KWANINI MAOMBI YA MACHOZI YAACHILIWE MAISHANI MWAKO Na Pastor GODLOVE INDIAEL


 

MAOMBI YA MACHOZI YANA ACHILIWA ILI YABEBE NINI ?

Sehemu ya 1.Yabebe vitu vya utukufu wa Mungu ndani MWAKO (maishani).

Yohana 11:1-4, 17, 19, 33-35,41-43

1 Basi mtu mmoja alikuwa hawezi, Lazaro wa Bethania, mwenyeji wa mji wa Mariamu na Martha, dada yake.

2 Ndiye Mariamu yule aliyempaka Bwana marhamu, akamfuta miguu kwa nywele zake, ambaye Lazaro nduguye alikuwa hawezi.

3 Basi wale maumbu wakatuma ujumbe kwake wakisema,  Bwana, yeye umpendaye hawezi.

4 Naye Yesu aliposikia, alisema, Ugonjwa huu si wa mauti, bali ni kwa ajili ya utukufu wa Mungu, ili Mwana wa Mungu atukuzwe kwa huo.

17 Basi Yesu alipofika, alimkuta amekwisha kuwamo kaburini yapata siku nne.

19 na watu wengi katika Wayahudi walikuwa wamekuja kwa Martha na Mariamu, ili kuwafariji kwa habari ya ndugu yao.

33 Basi Yesu alipomwona analia, na wale Wayahudi waliofuatana naye wanalia, aliugua rohoni, akafadhaika roho yake,

34  akasema, Mmemweka wapi? Wakamwambia, Bwana, njoo utazame.

35 Yesu akalia machozi

41 Basi wakaliondoa lile jiwe. Yesu akainua macho yake juu, akasema, Baba, nakushukuru kwa kuwa umenisikia.

42 Nami nalijua ya kuwa wewe wanisikia sikuzote; lakini kwa ajili ya mkutano huu wanaohudhuria nalisema haya, ili wapate kusadiki kwamba ndiwe uliyenituma.

43 Naye akiisha kusema hayo, akalia kwa sauti kuu, Lazaro, njoo huku nje.

Kuna vitu vinaachiliwa ndani ya Maisha yako ili utukufu wa Mungu uonekane ndani MWAKO .

Huyu ndugu Lazaro anaugua na kufa lakini kuugua kwake ni kwaajili ya utukufu wa Mungu .

0 comments: